Tuesday , 19 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Aibu Ikulu, Mtoto wa Rais ashikiliwa kwa utakatishaji fedha
Kimataifa

Aibu Ikulu, Mtoto wa Rais ashikiliwa kwa utakatishaji fedha

Dola za Marekani
Spread the love

VYOMBO vya dola nchini Angola vimemuweka kizuizini Jose Filomeno Dos Santos, mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Jose Eduardo Dos Santos kutokana na kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Mwana huyo wa rais anatuhumiwa kufanya utakatishaji fedha kiasi cha dola za kimarekani 500 milioni, fedha anazodaiwa kuzihamisha kinyume na sheria kutoka katika akaunti ya serikali kwenda kwenye akaunti binafsi ya benki ya Uswisi.

Kuchukuliwa hatua kwa Jose Filomeno ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Rais wa Angola, Joao Lourenco dhidi ya ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya wanafamilia ya rais mstaafu, Jose Dos Santos .

Ambapo mwezi Septemba mwaka jana alipoingia madarakani alimfukuza binti wa Jose Eduardo Dos Santos , Isabel Dos Santos katika wadhifa wa uenyekiti wa Kampuni ya Mafuta ya Sonangol inayomilikiwa na serikali.

Kabla ya Jose Filomeno kushtakiwa kwa kosa la ubadhirifu wa fedha, Rais Lourenco alimfuta kazi kwa kumuondoa katika Mfuko wa Serikali wenye zaidi ya dola za kimarekani 5 bilioni, ambapo alihudumu kama Mkuu wa mfuko huo, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa fedha.

Jose Filomeno alishitakiwa mwezi Machi 2018 katika mahakama nchini Angola kwa kosa la udanganyifu kuhusu usafirishaji wa fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Kimataifa

Tanzania, Italia kuimarisha ushirikiano sekta za kimkakati

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania na Italia zimeahidi kuimarisha ushirikiano katika...

Habari za SiasaKimataifa

Odinga avuka kihunzi cha kwanza uenyekiti AUC

Spread the loveAZMA ya kiongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

Kimataifa

‘Wachawi’ 50 wafariki baada ya kumeza dawa mitishamba

Spread the loveWatu zaidi ya 50 wanaoshutumiwa kwa ‘uchawi’ wamefariki dunia nchini...

error: Content is protected !!