Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

Ado Shaibu: Serikali ilitaka nimlipe Rais Milioni 123

Spread the love

ADO Shaibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema Serikali ilimtaka alipe Shilingi 123 Milioni kama faini ya kushindwa kesi aliyomshtaki Rais John Magufuli. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Katibu Mkuu huyo alimshtaki Rais Magufuli kwa kumteua Dk. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kudai kuwa kitendo hicho ni kinyume na katiba ya nchi kwakuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali anatakiwa kuwa amehudumu katika nafasi uwakili kwa muda wa miaka 10 hivyo Kilangi hakufikia hatua hiyo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi

Mahakama ilitupilia Mbali shauri hilo tarehe 20 Septemba mwaka 2019 ambapo Serikali iliiomba mahakama imuamuru alipe faini .

Leo tarehe 7 Juni 2020, Ado Shaibu amewaambia waandishi wa Habari kuwa Serikali iliiomba mahakama iamuru alipe kiasi cha shilingi 123 Milioni kama fidia kwa kushindwa kesi.

Ado ametanabaisha kuwa hatua hiyo ya serikali ilikuwa ikilenga kumkatisha tamaa yeye na wanaharakati wengine wenye kutaka kuiwajibisha serikali mahakamai kwa kutaka alipe kiasi kikubwa cha fedha kama fidia.

” Ili kunivunja moyo, Serikali imeomba fidia kubwa ya gharama ya kesi yangu kiasi cha shilingi 123,500,000 lakini bahati mzuri tarehe 3 Juni 2020, Mahakama imeniamuru kumlipa Rais Magufuli fidia ya Tsh. 445,000,”amesema Ado.

Ado amesema baada ya serikali kuona mahakama haitoshi imeamua kupeleka muswada wa sheria ya kuwakinga  bungeni.

ADO Shaibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema Serikali ilimtaka alipe Shilingi 123 Milioni kama faini ya kushindwa kesi aliyomshtaki Rais John Magufuli. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam...(endelea). Katibu Mkuu huyo alimshtaki Rais Magufuli kwa kumteua Dk. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kudai kuwa kitendo hicho ni kinyume na katiba ya nchi kwakuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali anatakiwa kuwa amehudumu katika nafasi uwakili kwa muda wa miaka 10 hivyo Kilangi hakufikia hatua hiyo. Mahakama ilitupilia Mbali shauri hilo tarehe 20 Septemba mwaka 2019…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!