Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ado ajitosa ukatibu mkuu ACT-Wazalendo
Habari za Siasa

Ado ajitosa ukatibu mkuu ACT-Wazalendo

Spread the love

KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amechukua fomu ya kugombea ukatibu mkuu wa chama hicho. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea). 

Akizungumza leo tarehe 20 Februari 2020, mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuchukua fomu hiyo, amesema amechukua fomu baada ya tafakuri ya kina na kwa kuzingatia maslahi mapana ya chama.

Aidha, ameeleza kuwa cheo cha ukatibu mkuu kwa chama hicho ni tofauti na vyama vingine vya siasa, CCM na vya upinzani ambapo ukatibu Mkuu wa ACT-Wazalendo ni wa kugombea.

Nafasi ya ukatibu mkuu katika chama hicho, unahitaji mwanachama kugombea na kisha kuchaguliwa na Halmashauri Kuu ya Chama.

“Binafsi nimefarijika kuona tayari wanachama wawili, Ndugu Dorothy Semu na Joran Bashange wamechukua fomu za kuwania nafasi hii. Wote wawili ninawafahamu vyema na ni watu ninaowaheshimu.

“Nina imani sisi watatu, iwapo tutateuliwa kuwa wagombea, tutaipa Halmashauri Kuu fursa ya kipekee ya kuchagua Katibu Mkuu bora anayeendana na wakati tunaoishi,” amesema na kuongeza;

“Tunaishi katika zama ambazo CCM inahofia sana uchaguzi, na inatamani kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kurudia uhuni walioufanya  kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tunahitaji Katibu Mkuu ambaye atafahamu kuwa huu ni mwaka wa maamuzi na hivyobasi yeye mwenyewe kuongoza programu za kuongoza umma kudhibiti uhuni huo.”

“Tunahitaji Katibu Mkuu ambaye ataelewa nafasi ya kipekee na ya kihistoria ya chama chetu katika kuhitimisha safari ndefu ya mapambano ya Wazanzibari katika kujikomboa. Tunahitaji Katibu Mkuu ambaye ataendeleza kwa kasi nafasi ya chama hiki kama ‘Sauti ya Wasio na Sauti’.

Ado amesema, nchi inapitia katika zama ambazo Watanzania wana kiu kubwa ya mabadiliko, na wameonesha mapenzi makubwa kwa ACT-Wazalendo kama mbadala wa uhakika.

“Wakati utapofika, kama nitafanikiwa kuteuliwa kuwa mgombea, nitaeleza kwa kina namna nilivyojipanga kuwa Katibu Mkuu bora na wa viwango kuendana na hali ya sasa.

“Kwa kuzingatia hoja hizo, na kwa kuwapima wenzangu, Dorothy Semu na Joran Bashange (na wengine wataojitokeza), nina imani kuwa Halmashauri Kuu ya chama itapata fursa muafaka ya kuchagua Katibu Mkuu anayefaa,” amesema. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!