Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Adakwa na doti 600 vitenge vyenye nembo ya CCM
Habari Mchanganyiko

Adakwa na doti 600 vitenge vyenye nembo ya CCM

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Shinyanga, inamshikilia mfanyabiashara Joseph Tasia akiwa na doti 600 za vitenge vyenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Takukuru imesema, vitenge hivyo vya kawaida, vinadaiwa kutaka kutumika kushawishi wapiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa tarehe 3 Julai 2020 na Mkuu wa Takukuru, Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa kupitia taarifa yake kwa umma.

         Soma zaidi:-

Mussa amesema, tarehe 29 Juni 2020 saa 3 usiku, katika mtaa wa Mwasele B nyumba ya Tasia, walimkuta na doti hizo za vitenge vikiwa vimehifadhiwa nyumbani kwake jambo ambalo linaashiria vilikuwa vinaandaliwa kutumika katika kufanya ushawishi kwa wapiga kura.

Amesema, uchunguzi walioufanya, wamebaini, Tasia ambaye ni mfanyabiashara wa usafiri wa magari madogo ‘taxi’ hana duka na wala hafanyi biashara ya kuuza vitenge.

“Katika mahojiano na maafisa wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, ameshindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na mzigo husika na hata nyaraka za manunuzi ya mzigo huo alizowasilisha hazijitoshelezi na hivyo kuongeza mashaka juu ya uhalali wa vitenge hivyo,” amesema Mussa.

Amesema, uchunguzi wa kina bado unaendelea ili kubaini iwapo vitenge vilikuwa ni kwa ajili ya kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa katika uchaguzi ujao au ni kwa ajili ya kufanya biashara msimu huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!