January 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo wakubali kuingia Ikulu Z’bar

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Spread the love

CHAMA cha ACT – Wazalendo, kimekubali kuungana na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), visiwani Zanzibar. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waadishi wa habari leo tarehe 6 Desemba 2020, jijini Dar es Salaam, Ado Shaibu ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho, amesema uamuzi huo uliofanywa na Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichoketi tarehe 5 Septemba 2020, umezingatia maoni ya baadhi ya wananchi, wanachama na viongozi wa chama hicho.

“Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya kufanya tadhmini ya kina, tumepata muda mrefu kufanya tafakuri ya kina, Kamati Kuu imesikiliza wanachama hasa walioathirika zaidi maoni yao, wameshirikishwa maoni ya viongoi wa chama.

“Kamati Kuu imeazimia wawakilishi wachache waliochaguliwa ambao ni madiwani, wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge waliotangazwa kushinda, waruhusiwe kushiriki kwenye vyombo vyao ili waendeleze mapambano,” amesema Ado na kuongeza:

“Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba yetu, imeridhia chama kushiriki kwenye Serikali ya Zanzibar na kupendekeza jina la Makamu wa Kwanza wa Rais.”

Amesema, uamuzi huo haukuwa mwepesi katika chama hicho na kwamba, hawaufurahii lakini walilazimika kuchagua kati ya uamuzi mbaya na uamuzi mbaya zaidi.

“Sio kwamba tunaufurahia uamuzi huu, tulikuwa njia panda kuchagua uamuzi mbaya ama uamuzi mbaya zaidi. Haikiwa chaguo baina ya uamuzi mzuri na mbaya bali mbaya au mbaya zaidi. Tumechagua njia ambayo ina nafuu katika kuendeleza mapambano,” amesema Ado.

 

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni baada ya siku kadhaa za giza, kutokana na chama hicho kuueleza umma kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu uliyofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Katika uchaguzi huo visiwani Zanzibar, Tume ya Uchaguzi visiw

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

ani humo ilimtangaza Dk. Mwinyi, aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushinda huku Maalim Seif Sharif Hamad wa Chama cha ACT – Wazalendo akitangazwa kushika nafasi ya pili.

Hatua ya kususia matokeo hayo ilitokana na kuwepo kwa malalamiko kwamba, uchaguzi huo uligubikwa na ulaghai hivyo  kusababisha ZEC kumtangaza mgombea wa CCM kushinda.

Miongoni mwa malalamiko yaliyoorodheshwa na chama hicho ni pamoja na kuenguliwa kwa wagombea wake kushiriki kwenye uchaguzi kinyume na taratibu, udanganyifu wakati wa utangazaji matokeo na kuwepo kwa kura feki.

Hata hivyo, ZEC ilikanusha madai hao huku ikisimamia kwamba, uchaguzi ulikuwa huru na haki na hakukuwa na kasoro za kufanya matokeo hayo yasiwe halali.

Wakati akitangaza baraza lake la mawaziri, Rais Mwinyi alisema, aliandika barua kwenda ACT – Wazalendo kuomba  jina la atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ambayo inaeleza, chama kitakachopata zaidi ya asilimia 10 ya kura za rais, kitashiriki kwenye serikali ya nchi hiyo, alikuwa hajajibiwa.

Siku moja baadaye, Maalim Seif akihojiwa na chombo kimoja nchini alisema, anasubiri uamuzi wa chama baada ya kufanya vikao vyao vya ndani ambao sasa umetangazwa leo.

error: Content is protected !!