Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo kuwa ‘Kanani ya Siasa’ 2020?
Habari za SiasaTangulizi

ACT-Wazalendo kuwa ‘Kanani ya Siasa’ 2020?

Bendera ya ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kinaweza kuwa nchi ya Kanani kwa wanasiasa kutoka kwa vyama mbalimbali vya nchini Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Kuna uwezekano mkubwa kuwa wanasiasa wakongwe na wenye mvuto kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  na wengi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) watahamia katika chama cha ACT-Wazalendo kutokana na sababu mbalimbali.

Sababu za wanasiasa kumtimka kutoka kwenye vyama vyao zinaweza kutofautiana kulingana lakini ufanano wao ni muelekeo wao utakuwa mmoja katika Chama cha ACT-Wazalendo ambayo kwao itakuwa kama Kanani ilivyokuwa kwa Wana wa Israel waliotoka utumwani nchini Misri.

Inaaminika kuwa kuna wanasiasa wengi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020 wapo watakaokwenda ACT-Wazalendo kimkakati kama inavyoaminika kwa sasa safari ya Edward Lowasa (Waziri Mkuu Mstaafu) ya Mwaka 2015 kutoka CCM kuhamia Chadema na kumpa karata ya turufu kugombea Urais na baadaye mwaka 2019 kurejea CCM.

Mkakati wa kisiasa utakaofanywa utakuwa na lengo la kwenda kudhoofisha kambi hiyo ili wakose nguvu kwenye mapambano ya 2020.

Wapo wanasiasa watakaikimbilia kambi hii kwa ajili ya kutafuta mustakabali wao wa kisiasa hasa ukizingatia kuwa kule kwenye vyama vyao mambo yashaharibika.

Mathalani, kovu lilioachwa na Maalimu Seif Sharif Hamad kwenye Chama cha CUF, kutokana na mgogoro wa muda mrefu ambao suluhu yake ilitolewa na Mahakama tarehe 18 Machi, 2019, ilipoamua kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa chama hicho.

Uamuzi huo wa Mahakama ulikinufaisha chama cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini, kwa kupata mtaji wa mwanasiasa mkongwe mwenye mvuto visiwani Zanzibar na maelfu ya wafuasi wa CUF.

Maalim Seif ambaye ni Mshauri mkuu wa ACT-Wazalendo amekiongezea mvuto chama hicho ambacho kishajiwekea mizizi visiwani Z’bar na kwamba kwa sasa kimekuwa tishio Bara.

Ithibati ya kuwa chama hiki kimekuwa tishio kwa sasa  kutokana na vikwazo vya waziwazi vya kisiasa licha ya kuwepo kwa zuio liliwekwa na Serikali la kufanya mikutano ya nje kwa vyama vyote vya siasa nchi mpaka wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wabunge kadhaa wa chama cha CUF hawajaweka wazi msimamo wao juu hatma yao ya kisiasa ndani ya chama hicho  licha ya kufahamika kwa wabunge wachache waliibuka waziwazi kumuunga mkono Profesa Lipumba kama vile Maftaha Namchuma, Hamidu Bobali Mbunge wa Mchinga.

Zipo taarifa zinazotoka kwenye chanzo cha uhakika kuwa wabunge wengi wa CUF watatimkia ACT-Wazalendo ifikapo 2020 kinachowashughulisha ni kuacha ubunge wao wakati wamebakiza muda mchache kustaafu.

Wabunge hao wanaaonyesha kuwa wanasubiri tu muda wa kumaliza ubunge wao wakiwa CUF, lakini wanaweza kumfuata Maalim Seif ndani ya ACT-Wazalendo ili kuendeleza na itikadi zao kama walivyokuwa ndani ya chama chao.

ACT-Wazalendo wanaweza kuvuna vigogo ndani ya CCM kutokana na kuwepo kwa mvutano wa chini chini ulikuwepo ndani ya chama hicho kutokana na kupokelewa kwa wapizani na kupewa madaraka.

Mashaka hayo yameanza baada ya baadhi ya wanachama hayo kuanza kukacha mafundo ya itikadi kwa wanasiasa hao yanaanza kuonekana pale wanapoanika maumivu yao kwenye mitandao ya kijamii kana kwamba usuluhishi wa ndani umegonga mwamba.

Wafuasi wa chama hicho wanaonekana kukichoka kutokana na minyukano ya ndani mathalani, ule mnyukano uliowakabili wabunge wanaotoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Mnyukano mwingine unaoweza kuibuka ndani ya nyoyo za wanaCCM kutokana na wageni waliotoka kambi ya upinzani nafasi hasa zile za uteuzi kama ule wa Patrobas Katambi, David Kafulila, Anna Mngwira, Profesa Kitila Mkumbo na wengine.

Mbali na CCM na CUF lakini ACT-Wazalendo wanaweza kuvuna vigogo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutokana ndani huko kuwa na mgogoro unaowagawa wavunge na viongozi ndani ya chama hicho.

Wabunge kama Mwita Waitara ambaye kwa sasa ni Mbunge wa CCM na Naibu Waziri alikihama chama hicho na kurudi CCM kutokana na mvutano wa ndani ya chama hicho.
Mwita alidai ameondoka ndani ya Chadema kutokana na yeye kuhoji juu ya madaraka ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambaye anataka kuendelea kukiongoza chama hicho huku baadhi yao wakiona kuwa hana uwezo wa kuendelea kuwa mwenyekiti.

Mbunge huyo wa Ukonga, alidai kuwa kuna watu wengi sana tena wabunge ambao wanapinga Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti na wanaompinga wanaweza kuondolewa katika nafasi za kugombea tena ubunge.

Kama kweli kuna wabunge ambao wanaweza kutemwa katika nafasi zao za kugombea ubunge watakimbilia ACT-Wazalendo kutokana na chama hicho kuwa na mvuto na kinatarajiwa kuwa chama kikubwa cha upinzani baada ya uchaguzi wa 2020.

Muda utaongea. Mengi yatatokea katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!