Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo kujadili uundwaji Serikali Z’bar 
Habari za SiasaTangulizi

ACT-Wazalendo kujadili uundwaji Serikali Z’bar 

Kaimu Naibu Katibu Mkuu ACT-Wazalendo-Zanzibar, Salim Bimani (Picha na Mintanga Hunda)
Spread the love

CHAMA cha siasa cha upinzani nchini Tanzania, ACT-Wazalendo kimesema, kitafanya vikao kwa ajili ya kujadili  kama kitashiriki katika uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani Zanzibar au hakitashiriki. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 6 Novemba 2020 na Kaimu Naibu Katibu Mkuu ACT-Wazalendo-Zanzibar, Salim Bimani alipoulizwa na MwanaHALISI Online juu ya msimamo wa chama hicho katika kuunda serikali hiyo.

Bimani amesema vikao hivyo vitafanyika ndani ya mwezi huu, baada ya vikao vya kutathimini athari zilizotokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 kumalizika.

“Sasa hivi chama kimekaa kinashughulikia masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu. Kikao cha kamati kuu kinafanyika kushuhghulikia masuala ya maafa, kikao kinachofuata tutajadili suala hilo. Kwa sasa hatujajadiliana juu ya watu wengi walioumia na waliokuwepo vizuizini,” amesema Bimani.

Bimani amesisitiza, “kuhusu kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, vikao vya chama ndio vyenye maamuzi. Tusubiri maamuzi yake.”

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Chama kinachoshinda Uchaguzi Mkuu wa Urais visiwani humo na kinachoshika nafasi ya pili kwa wingi wa kura, vinaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kuwapo na makamu wawili wa Rais.

Makamu wa kwanza wa Rais anatokana na chama kilichoshika nafasi ya pili na makamu wa pili wa Rais anatokana na chama tawala.

Utekelezaji wake ulifanyika kwa kipindi kimoja kati ya mwaka 2010-2015 ambapo, Maalum Seif Sharif Hamad alikuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) ambapo Maalim Seif alikuwa makamu wa kwanza wa Rais na Balozi Seif Ali Iddi akiwa makamu wa pili wa Rais huku Rais akiwa Dk. Ali Mohamed Shein.

Pia, mawaziri na naibu mawaziri walitokana vyama hivyo vya CCM na CUF.

Mwaka 2015, CUF hakikubali kushiriki katika uchaguzi wa marudio baada ya ule wa awali kufutwa hivyo kupoteza sifa za kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa hivyo nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais kutokuwa na mtu.

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi alitangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar humo (ZEC), baada ya kupata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27

Huku aliyekuwa mpinzani wake wa karibu kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akishika nafasi ya pili baada ya kupata kura 99,103 sawa na asilimia 19.87.

Hata hivyo, ACT-Wazalendo na Chadema kwa pamoja vimetangaza kutoyatambua matokeo ya uchaguzi mkuu uliosimamiwa na ZEC upande wa Zanzibar na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) upande wa Tanzania Bara.

Vyama hivyo kwa pamoja, vinataka uchaguzi huo uliomwingiza madarakani Rais Mwinyi na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ufutwe na uitishwe upya kwa kutumia Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!