Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa A-Z kuapishwa Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

A-Z kuapishwa Magufuli

Spread the love

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma, amemwapisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania atakayeongoza Taifa hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2020-2025). Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Dk. Magufuli ameapishwa leo Alhamisi saa 4:07 asubuhi tarehe 5 Novemba 2020 katika sherehe iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Rais Magufuli ameapishwa siku na tarehe kama ya leo aliyoapishwa katika ungwe yake ya kwanza ya miaka mitano tarehe 5 Novemba 2015 akipokea kiti kutoka kwa Rais aliyemwachia wadhifa huo, Jakaya Mrisho Kikwete.

Sherehe hizo zimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dodoma, Makao Makuu ya Tanzania. Ikumbukwe, watangulizi wake wote wanne, waliapishwa katika Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao wamehudhulia sherehe hizo zilizopabwa na gwaride maalum la vikosi vya ulinzi na usalama.

Pia, mawaziri, naibu mawaziri, katibu wakuu na naibu wao, wakuu wa mikoa, wilaya, wakuu wa mashirika na taasisi za umma, wabunge wateule na wale waliomaliza muda wao, viongozi wa dini na baadhi ya waliokuwa wagombea urais walikuwepo.

Ni marais wanne wamehudhulia sherehe hizo ambao ni; Yoweri Mseveni (Uganda), Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe), Azali Assoumani (Comoro) na Dk. Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar.

Wengine ni, marais wastaafu Olusegun Obasanjo wa Nigeria na Sylvester Ntibantunganya wa Burundi ambaye alikuwa mwakilishi wa waangalizi wa uchaguzi huo kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pia, Marais wastaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Ali Hassan Mwinyi. Pia, marais wastaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Aman Abeid Karume.

Wengine ni; Mohamed Gharib Bilal, makamu wa Rais mstaafu wa Tanzania amehudhulia hafla hiyo wakiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu waliohudhulia ni; Jaji Joseph Warioba, Mizengo Pinda, Edward Lowassa na Cleopa David Msuya.

Baadhi ya wagombea urais waliochuana na Rais Magufuli katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano tarehe 28 Oktiba 2020 wamehudhulia ambao ni; Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini), Queen Sendiga (ADC) na Muttamwega Mgaya wa SAU.

Alivyoingia uwanjani

Saa 3:44 asubuhi, msafara wa magari na pikipiki uliokuwa umembeba Rais John Pombe Magufuli uliingia akiwa katika gari la wazi akiwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo na kuibua shangwe uwanja mzima wakipeperusha bendera za Tanzania walizozishika mkononi.

Msafara huo, ulizunguka uwanja mzima wa Jamhuri huku akiwa anawapungua mkono wa kuwasalimia huku ulinzi ukiwa umeimalishwa vilivyo.

Saa 3:48 asubuhi, alishuka katika gari la wazi na kwenda moja kwa moja katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kupokea heshima kwa Rais ikiwemo kuimba wimbo wa Taifa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiambatana na mizinga 21.

Saa 3:54 asubuhi, baada ya kuhitimisha heshima hiyo, Rais Magufuli alilikagua gwaride hilo na kurejea eneo maalum alilofikia.

Bendera yashushwa

Saa 4:01 bendera ya Rais ya Tanzania ilishushwa ikiashilia kuondoka kwa madaraka yake ya urais ikiwemo baraza lake la mawaziri kumalizika muda wake.

Wakati huo, Dk. Magufuli alibaki na wadhifa wa Rais mteule pekee huku nchi ya Tanzania ikiwa chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Saa 4:05, Rais mteule Magufuli, alishuka eneo hilo na kwenda jukwaani kwa ajili ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambako kwenye jukwaa hilo alikuwepo makamu wa Rais mteule, Samia Suluhu Hassan.

Saa 4:07 asubuhi, Rais mteule wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliombwa kusogea katika meza ya kiapo.

Saa 4:07 asubuhi, Dk. John Pombe Magufuli aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania.

Saa 10:10 asubuhi, alimaliza kula kiapo kisha kukisaini na kusainiwa pia na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Samia Suluhu Hassan

Saa 4:11 asubuhi, Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Saa 4:13 asubuhi, Samia Suluhu Hassan alimaliza kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania na kusaini kiapo hicho

Saa 4:15 asubuhi, Rais Magufuli alikwenda kukaa kiti cha jadi kisha kukabidhiwa mkuki na ngao kisha zilifuatia dua kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini akiwemo; Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ally na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Gervas Nyaisonga.

Saa 4:31 asubuhi, shughuli ilimalizika ya uapisho ambapo wazee wa Tanzania Bara na Zanzibar, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan walikwenda jukwaa kuu walikokaa viongozi mbalimbali.

Bendera yapandishwa

Saa 4:39 asubuhi, alikwenda eneo maalum lililoandaliwa ili kupigiwa heshima ya Rais iliyoambatana na wimbo wa Taifa na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na mizinga 21 huku  bendera ya Rais ikipandishwa.

Wakati huo, Rais Magufuli alibadilisha tai, awali, aliingia akiwa amevalia shuti nyeusi, shati nyeupe na taifa nyekundi lakini baada ya kuapishwa alibadilisha na kuvaa ya zambarau.

Baada ya wimbo huo, Gwaride maalum, lilijiumba katika umbo la alfa ambapo saa 4:47 asubuhi, Rais Magufuli alilikagua likiwa na ishara ya mwanzo wa ungwe ya pili ya miaka mitano 2020-2025.

Saa 4:53 alimaliza kukagua na kupanda jukwaani ambako alisalimiana na marais na wageni mbalimbali waliohudhulia shughuli hiyo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbalui

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!