March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Z’bar imerejea ‘gizani’ ’

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeeleza, uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, umerejesha visiwa hiyo ‘gizani’. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akieleaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho cha ACT-Wazalendo kuhusu ushiriki wake kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Ado Shaibu ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho leo tarehe 6 Desemba 2020, amesema siasa za chuki zimerejea visiwani humo.

“…hivi sasa ambapo siasa za chuki na uhasama zimerudi upya kutokana na makovu yanayotokana na uchaguzi wa Mwaka 2020. Kwamba Zanzibar inahitaji busara kubwa katika kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi huo.

“Pia, Zanzibar inahitaji hekima na busara katika kuhakikisha kuwa matukio ya namna hii hayajirudii tena na kwamba, lazima kuwe na utaratibu wa kuhakikisha kuwa chaguzi zijazo zinakuwa huru, za haki, zinazokubalika na zenye hali ya utulivu,” amesema Ado wakati akiwaambia waandishi uamuzi wa chama hicho kushiriki kwenye Serikali ya Zanzibar.

Akisoma maazimio hayo, Ado amesema Zanzibar imekuwa ikigubikwa na hali iliyojaa majeraha, uhasama mkubwa wa kisiasa na hata watukuuana baada ya uchaguzi.

Amesema, hali hiyo iliyokuwa ikitokea awali sasa imerejea tena baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba, inahitajika busara kutibu majeraha hayo.

“Historia ya kisiasa ya Zanzibar kwa kila uchaguzi tangu Uhuru na hata baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, imekuwa ikigubikwa na hali iliyojaa majeraha, uhasama mkubwa wa kisiasa, watu kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa, kudhalilishwa kijinsia na mali za watu kuharibiwa.

“Hali hii imejirudia tena katika uchaguzi wa mwaka 2020, kutokana na madhila ya uchaguzi huu ikiwemo kupigwa risasi, vipigo na mashambulizi ya kimwili, watu wamejeruhiwa na wengine kudhalilishwa kijinsia na mali zao zikiharibiwa na kuibiwa,” amesema Ado na kuongeza:

“Wakati pekee ambao Zanzibar imefanya uchaguzi wa kistarabu na wananchi  kusalimika na maafa pamoja na madhila yanayotokana na uchaguzi katika historia ya chaguzi Zanzibar, ni kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo Zanzibar ilikuwa imeingia katika  Maridhiano ya Novemba 5, 2009 kabla ya uchaguzi huo.

“Pia katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambao ulikuwa ni uchaguzi bora kuliko chaguzi zote kabla ya kufutwa kwake. Uchaguzi huu nao ulifanyika wakati ambapo Zanzibar ilikuwa ipo chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ni zao la Maridhiano.”

error: Content is protected !!