April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi wa dini kuiombea Lipuli isishuke Ligi Kuu

Spread the love

VIONGOZI wa dini mkoani Iringa wameombwa kuiombea timu ya Lipuli FC ili isiweze kushuka daraja, katika kipindi cha siku 14 ambapo timu hiyo itacheza michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara ili kuhakikisha inafanya vizuri na kubakiwa kwenye Ligi hiyo kwa msimu ujao. Anaripoti Mwandishi wetu… endelea

Akizungumza na wanahabari kwa niaba ya kamati ya kusaidia timu hiyo isishuke daraja, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Abuu Changawa amesema kuwa ni jukumu la kila mkazi wa Iringa kuisapoti timu hiyo ili kuhakikisha mechi zilizobaki wanafanya vizuri.

“Kama wachezaji wakiishusha timu kutakuwa hakuna lawama lakini sisi kama wanairinga tukijitokeza kuwaunga mkono,tukaingia uwanjani kuwashangilia kila mchezaji atapata faraja”.

“Kuanzia kesho mageti yatakuwa wazi kuanzia saa nane mchana nawaomba wanairinga wajitokeze kwa wingi tuishangilie timu yetu,madhaifu na mapungufu yaliyopo katika uongozi sio mahara pake,tukimaliza ligi tutakaa tuangalie tulijikwaa wapi tusonge mbele”alisema Changawa.

Kiongozi huyo aliongezea kuwa timu hiyo inaweza kuwa inakutana na changamoto ndogondogo kwa sasa licha ya kuanza vizuri ligi ilipoanza na kuahidi kuwa kwa sasa watashirikiana na kamati tendaji ya Lipuli kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.

Lipuli kwa sasa imebakiza michezo minne kwenye Ligi Kuu Tanzania bara, ikiwa na pointi 37, huku ikishika nafasi ya 18 kwenye msimamo na siku ya kesho  itashuka dimbani dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Samora, huku wakijiandaa kuwakabili klabu za Ruvu shooting, Azam Fc na mchezo wa mwisho utakuwa dhidi ya Yanga.

 

error: Content is protected !!