Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko BoT yashusha ahueni kwa wakopaji
Habari MchanganyikoTangulizi

BoT yashusha ahueni kwa wakopaji

Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Spread the love

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imezitaka benki na taasisi za fedha nchini humo, kutoa unafuu wa urejeshaji mikopo, ili kupunguza makali ya athari za janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19), kwa wateja wake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 12 Mei 2020 na Prof. Florens Luoga, Gavana wa BoT, wakati akitangaza maazimio ya kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha ya benki hiyo, kuhusu athari za Covid-19 katika uchumi, kilichofanyika tarehe 8 Mei 2020.

Tanzania iliripoti kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa Covid-19 tarehen 16 Machi 2020, kisha kesho yake yaani tarehe 17 Machi 2020, Serikali kupitia Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu, ilitangaza marufuku ya shughuli zinazohusisha mikusanyiko ya watu wengi.

Tanzania kama ilivyo nchi nyingine duniani,  imeathirika kiuchumi  kutokana na janga la Corona huku sekta ya utalii, elimu na shughuli za kijamii zikiathirika zaidi,  baada ya kusimama kutokana na katazo la mikusanyiko ya watu wengi.

Katika taarifa yake, Prof. Luoga amesema kamati hiyo imezishauri benki na taasisi za fedha, kujadiliana na wakopaji, kuhusu namna ya kurejesha mikopo kulingana na athari za Covid-19 katika shughuli zao.

“Hatua za kisera zilizopitishwa ni, benki na taasisi za fedha kutathimini kwa kina athari zinazotokana na mlipuko wa Covid-19, kwenye urejeshaji wa mikopo, kujadiliana na wakopaji namna ya kurejesha mikopo. Na Kutoa unafuu wa urejeshaji wa mikopo itakavyoonekana inafaa,” inaeleza taarifa ya Prof. Luoga.

Kuhusu hatua nyingine tano za kisera kwa ajili ya kukabiliana na athari za mlipuko katika uchumi zilizochukuliwa na BoT, Prof. Luoga amesema hatua ya kwanza ni ushushaji kiwango cha chini cha kisheria cha sehemu ya amana kutoka asilimia 7 hadi kufikia 6, kinachotakiwa kuwekwa BoT.

Hatua ya pili ni, ushushaji wa kiwango cha riba kinachotozwa kwa benki inapokopa BoT, kutoka asilimia 7  hadi kufikia asilimia 5.

“Hatua hii itawezesha kuongeza wigo wa benki kukopa kutoka kwa benki kuu kwa riba nafuu, na hivyo kupunguza riba ya mikopo kwa wateja,” inaeleza taarifa ya Prof. Luoga.

Prof. Luoga amesema hatua ya tatu iliyochukuliwa ni,  BoT kuongeza unafuu kwenye dhamana na hati fungani za serikali zinazotumika na benki kama dhamana,  wakati wa kukopa kutoka katika benki hiyo.

Akizungumzia hatua hiyo, Prof. Luoga amesema itasaidia kupunguza kiwango cha dhamana kutoka 10% hadi 5%, kwa dhamana za muda mfupi, na 40% hadi 20% kwa hati fungani, hali itakayoongeza uwezo wa benki kukopa kutoka BoT.

Hatua ya nne, iliyochukuliwa na BoT ili kufidia athari za Covid-19 katika uchumi, ni kampuni zinazotoa huduma za fedha kwa njia ya mtandao kuongeza kiwango cha miamala kwa mteja kwa siku, kutoka Sh. 3 Mil. hadi Sh.5 Mil.

“Makampuni yanayotoa huduma za fedha kwa njia ya mtandao kuongeza kiwango cha miamala kwa siku kwa mteja kutoka Sh. 3 Mil. hadi Sh. 5 Mil, na kiwango cha akiba kwa siku kwa mteja kutoka Sh. 5 Mil. hadi Sh. 10 Mil,” inaeleza taarifa ya Prof. Luoga.

Prof. Luoga amesema hatua hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha za kidigitali kwenye miamala mbalimbali, na kupunguza ulazima wa wateja kwenda benki.

“Aidha, mabenki yamehimizwa kuongeza matumizi ya mifumo ya kufanya miamala kwa njia ya kidigitali, ikiwemo matumizi ya mashine za kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki za kibenki,” inaeleza taarifa ya Prof. Luoga.

Hatua ya mwisho iliyochukuliwa na BoT ni, kuendelea kufanya tathimini ya athari za mlipuko wa ugonjwa huo katika sekta mbalimbali za uchumi, kwa lengo la kuchukua hatua stahiki ili kupunguza madhara ya athari hizo.

Prof. Luoga amesema hatua hizo zimeanza kutekelezwa leo tarehe 12 Mei 2020.

Wakati huo huo, Prof. Luoga amesema Tanzania ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, zenye uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!