Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Marufuku kuuza chakula, matunda karibu ya vyoo
Habari Mchanganyiko

Marufuku kuuza chakula, matunda karibu ya vyoo

Dk. Gatete Mahava, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Spread the love

MGANGA Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Gatete Mahava ametoa onyo kwa wafanyabiashara wote wanaouza chakula au matunda karibu na vyoo chini ya mita 30 na kuwataka waondoe biashara zao mara moja. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo ametoa agizo kwa Afisa Afya wa Jiji la Dodoma, Abdallah Mahia kuahakikisha anafanya msako wa kuwabaini watu wote wanaofanya biashara ya chakula na matunda katika milango ya vyoo katika stendi ya daladala ya Sabasaba na soko la Sabasaba.

Dk. Mahava ametoa agizo hilo baada ya mama lishe pamoja na wauzaji wa matunda wanafanyabiashara zao karibu na milango ya vyoo jambo ambalo linaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa huku asifa Afya akiwa mzito kutoa ushirikiano na mwandishi wa habari.

Alisema utaratibu unaotakiwa kufanyika ni kwamba vyoo vya jumuiya vinatakiwa kujengwa angalau hatua 30 japo inategemeana na mazingira huku akitoa mfano wa vyoo vya nyumbani kuwa haviwezi kujengwa hivyo, lakini sehemu zenye mkusanyiko kama ilivyo soko la Sabasaba ambapo kuna na stendi hauwezi kujenga vyoo ambavyo watu wanafanyabiashara milangoni.

“Kwa sasa mvua zinaendelea kunyesha na kuna uwezekano mkubwa nzi akatoka chooni na kuingia katika chakula au katika matunda jambo hilo linaweza kusababisha kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko, kutokana na hali hiyo sasa kuanzia leo nimemuagiza Afisa Afya wa Jiji pamoja na timu yake kuhakikisha wanafanya msako na kubaini vilipo vyoo ili wanaofanya biashara katika maeneo hayo wafunge na wabadilishe biashara na isiwe biashara ya matunda wala chakula,” alisema Dk. Mahava.

Aidha alisema kuwa imekuwepo changamoto katika maeneo ya stendi ya daladala ya Sabasaba  na sehemu nyingine yenye mikusanyiko kuwa na tabia ya watu kuuza vyakula au matunda karibu na vyoo, sasa napenda kutoa onyo kwa wale wanaouza vyakula karibu na vyoo vya jumla, kwa kawaida unatakiwa kuuza vyakula au matunda takribani mita 30 toka kwenye vyoo.

Dk. mahava alisema kuwa kwa kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha katika jiji la Dodoma kunahitajika umakini wa hali ya juu zaidi katika kufanya usafi ili kuondokana na milipuko ya magonjwa ambayo inaweza kujitokea.

Katika hatua nyingine Dk. Gatete, amesema kuwa halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa sasa inafanya utaratibu wa kuboresha stendi ya Sabasaba na soko hilo ili kuona ni jinsi gani wataweza kujenga vyoo vya kisasa ambavyo vitakuwa vinajitegemea, sehemu maalum ya kuuzia nguo za mitumba, matunda na mbogamboga pamoja na vyakula kwa ujumla na kueleza kuwa kwa sasa umeanza uboreshaji wa Stendi ya daladala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!