Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Mkuu mgeni rasmi Mviwata
Habari Mchanganyiko

Waziri Mkuu mgeni rasmi Mviwata

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Khasim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) yatakayokuwa na kutaniko la wakulima takriban 2400. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mkurugenzi wa MVIWATA, Stephen Ruvuga alisema hayo jana mbele ya waandishi wa Habari na kwamba Waziri Mkuu atafungua maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais John Magufuli na kwamba maadhimisho hayo yatafanyika Oktoba 3 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Ruvuga alisema, maadhimisho hayo yatafuatiwa na kongamano la kitaifa la wakulima lenye mada inayohusu “ujenzi wa uchumi wa viwanda nini nafasi ya wakulima wadogo” likifuatiwa na Mkutano Mkuu wa 23 wa MVIWATA vitakavyofanyika Oktoba 4- 5 katika ukumbi uliopo kwenye Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro (MUM).

Aidha alisema, Rais Magufuli pia amemtuma mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dk. Bashiru Ally ambaye atakuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo licha ya kushiriki kuanzia kwenye maadhimisho.

Alisema Kongamano hilo litajadili jinsi gani wakulima wanaweza kujipanga na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na kuangalia viwezeshi muhimu vya kufanikisha ushiriki wa kweli wa wakulima wadogo katika mfumo wa uchumi wa viwanda ambao ndiyo mkakati wa Serikali ya awamu ya tano.

Mkurugenzi huyo alisema, Katika kongamano hilo licha ya kuwa na watoa mada wengine Dk. Bashiru Ally atakuwa ni mtoa mada mkuu na kwamba amekuwa ni mchambuzi wa masuala ya uchumi, siasa na jamii kwa muda mrefu ambaye ana imani atatoa maoni yatakayotoa mwelekeo wa ujenzi wa uchumi wa viwanda na CCM kama chama kinachoongoza Serikali kinavyowatazama wakulima.

Naye Afisa Ushawishi na Utetezi kutoka MVIWATA, Thomas Laizer alisema licha ya wanachama wa MVIWATA kushiriki, tukio hilo linategemewa kuhudhuriwa na wageni kutoka Nyanja mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Viongozi na Watendaji waandamizi wa Serikali, Wawakilishi wa Balozi, Washiriki Wenza, Marafiki wa MVIWATA na wadau wengine kutoka ndani na nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!