Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Bobi Wine akamatwa tena, apelekwa pasipojulikana
KimataifaTangulizi

Bobi Wine akamatwa tena, apelekwa pasipojulikana

Spread the love

MBUNGE wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama ‘Bobi Wine’ amekamatwa na Jeshi la Polisi alipowasilisi katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe akitokea nchini Marekani alikokuwa anapatiwa matibabu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Polisi nchini humo wamenukuliwa na vyombo vya habari wakisema kuwa, Bobi Wine hajapewa kibali cha kufanya mkutano au shughuli yoyote, ambapo  Msemaji wa polisi mjini Kamapala, Luke Owoyesigyire, alionya kuwa yeyote atakayeshiriki kwenye shughuli yoyote inayomhusu Bobi Wine atakamatwa.

Hadi sasa inadaiwa ndugu wa Bobi Wine anayefahamika kwa jina la Eddy Yawe na Naibu Msemaji wa chama cha Democratic Party, Waiswa Alex Mufumbiro, walikamatwa na vikosi vya usalama na kuzuiwa kwenye kituo cha polisi uwanja wa Entebbe.

Vile vile, Jeshi la Polisi nchini humo limesambaza askari polisi kwenye barabara ya kutoka Kampala kuelekea Entebbe, ambayo inasadikika wafuasi wa Bobi Wine watakusanyika kumpokea mbunge huyo.

Bobi Wine anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kufuatia tuhuma za kuhusika katika tukio la kupigwa mawe msafara wa Rais Yoweri Meseveni wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!