Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

‘2020-2025 ajira mil 8, ndege tano, meli nane’

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amesema, mpaka kufikia mwaka 2025, atahakikisha amenunua ndege tano ikiwemo ya mizigo, meli nane za uvuvi pamoja na kupatikana ajira za watu milioni nane. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza kwenye Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020, Rais Magufuli amesema, anachukua hatua hizo ili Watanzania wengi wawe mabilionea.

Huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema “tunahitaji kuwa na mabilionea wengi wa Kitanzania wakiwemo wabunge. Nataka Watanzania wote washiriki kikamilifu katika kujenga nchi yao.”

Katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, Rais Magufuli ameihamishia Ofisi ya Rais kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Uwekezaji “ili hao wanaokwamisha nikapambane nao mimi mwenyewe. Nataka mwekezaji mwenye fedha zake, akija apate kibali ndani ya siku 14.”

Rais John Magufuli

“Miaka mitano ijao tunakusudia kununua ndege tano ikiwemo moja ya mzigizo ili kurahisisha usafirishaji minofu ya nyama na mazao ya bustani.”

“Wakulima wetu wafaidike na shughuli wanazozifanya,” amesema Rais Magufuli na kuongeza “katika miaka mitano ijayo, tutatoa ajira mpya milioni nane.”

Amesema, miongoni mwa mambo anayoyapa kipaumbele katika miaka mitano ijayo ni pamoja na kuendelea kulinda na kudumisha tunu za Taznania ikiwa pamoja na amani, umoja na mshikamano.

“Naahidi kushirikiana na Dk. Mwinyi (Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar), kamwe hatutakuwa na mdhaha na yeyote anayetaka kuhatarisha amani ya nchi yetu.”

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Amesema, anakusidia kuimarisha utawala bora, kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma, kukabiliana na wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.

“Watumishi wazembe bado wapo, walarushwa, wezi, wala mali bado wapo. Miaka mitano ijayo tutawashughulikia, kwa kifupi niseme utumbuaji utaendelea,” amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa

“Tutaendelea kuboresha mazingira ya kazi pamoja na maslahi ili yaendane na utumishi. Watumishi wasiwe na wasiwasi, wachape kazi. Miaka mitano ijayo tumejipanga kuendeleaza jitihada za kuendeleza na kukuza uchumi,” amesema.

Rais Magufuli amesema, amekusudia kununua meli nane za uvuvi ambapo mbili zitatumika upande wa Tanzania Bara na mbili zitatumika kwa uapande wa Zanzibar.

“Tumepanga kununua meli nane za uvuvi, meli nne zitatumika Bara nan ne zitatumika Zanzibar. Meli hizo zitashiriki katika uvuvi wa bahari kuu, suala la uvuvi ni la muungano. Tutahamasisha sekta binafsi kujenga viwanda vya kuchakata samaki,” amesema.

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amesema, mpaka kufikia mwaka 2025, atahakikisha amenunua ndege tano ikiwemo ya mizigo, meli nane za uvuvi pamoja na kupatikana ajira za watu milioni nane. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). Akizungumza kwenye Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020, Rais Magufuli amesema, anachukua hatua hizo ili Watanzania wengi wawe mabilionea. Huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema “tunahitaji kuwa na mabilionea wengi wa Kitanzania wakiwemo wabunge. Nataka Watanzania wote washiriki kikamilifu katika kujenga nchi yao.” Katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, Rais Magufuli ameihamishia Ofisi ya Rais kutoka…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!