Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ATCL yaanza kutikisa anga za kimataifa
Habari za SiasaTangulizi

ATCL yaanza kutikisa anga za kimataifa

Spread the love

KAMPUNI ya ndege ya taifa (ATCL), leo Alhamisi ya tarehe 30 Agosti 2018, inatarajiwa kuzindua safari yake ya tatu ya kimataifa, itakayoanzia Dar es Salaam kuelekea Bunjumbura nchini Burundi. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya ATCL jijini Dar es Salaam, wizara ya mawasiliano na uchukuzi na ubalozi wa Tanzania nchini Burundi zinasema, ndege ya kwanza ya shirika hilo, inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam saa 3:30 na kutua mjini Bujumbura, majira ya saa 5:40 asubuhi.

Tayari ATCL imezindua safari nyingine mbili za kimataifa zinazoanzia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), kuelekea Entebe nchini Uganda na Comoro.

“…jambo Burundi,” ndivyo moja ya kipeperushi cha shirika hilo ambacho MwanaHALISI Online inacho, kinavyosema kuelezea uzinduzi wa safari yake hiyo nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kwa kuanzia ATCL itatumia ndege yake aina ya Bombardier Dash 8 Q400 katika safari hiyo. Ndege hiyo itaelekea Bujumbura, kupitia Kigoma nchini Tanzania.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ya uzinduzi, ni pamoja na wabunge watatu wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, wakiongozwa na Daniel Nsanzungwanko.

Wengine watakaohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi, ni Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Injinia Isaack Kamwele; Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Gervais Abayeho; Mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi; Meneja Masoko na Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Edward Nkwabi na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Elias Kwandikwa.

ATCL iko katika mapambano ya kurejesha huduma zake, kufuatia “kuuawa” na tawala za marais waliopita, Benjamin William Mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Uchambuzi kamili juu ya ATCL inakotoka, inakoelekea na changamoto zake, soma MwanaHALISI Online Jumapili hii – Mhariri. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!