Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 169 udiwani CCM wapeta Kilimanjaro
Habari za Siasa

169 udiwani CCM wapeta Kilimanjaro

Spread the love

WAGOMBEA udiwani 169 kati ya 1145 ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), walioomba kuteuliwa kugombea udiwani kupitia chama hicho mkoani Kilimanjaro, wamepitishwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).

Majina ya madiwani hao yametangaza rasmi jana tarehe 17 Agosti 2020 na Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani humo baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa.

”Wagombea hawa 169 ndio waliopendekezwa na kuteuliwa na kikao cha Halmashauri Kuu kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,” amesema na kuongeza:

”Ni dhahiri kuwa, mchakato wetu wa kikatiba na kikanuni uliendelea baada ya kura za maoni kupigwa. Vikao vya uchujaji  na utoaji mapendekezo viliendelea ambapo kamati zote za siasa kuanzia kata hadi mkoa zilikaa na kutoa maoni na mapendekezo yake.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!