Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 16 kuchuana ubunge Arusha Mjini
Habari za Siasa

16 kuchuana ubunge Arusha Mjini

Spread the love

WAGOMBEA 16 wa vyama vya siasa nchini Tanzania, watachukuana kuwania Ubunge wa Arusha Mjini katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Wagombea hao, wameteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo Arusha Mjini, Dk John Pima.

Walioteuliwa ni mbunge anayetetea nafasi hiyo, Godbless Lema wa Chadema na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anayegombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Leman na Gambo wanatarajia kuchuana kuwania uwakilishi wa wananchi hao wa Arusha Mjini.

Wagombe wengine ni; Zuberi Mwinyi (ADA- TADEA), Shayo John (ACT- Wazalendo), Husna Kundi(AAFP), Matayo Richard (CCK), Magdalena Shanghai (CUF), Elisante Mjema (Demokrasia Makini), Elizabeth Godfrey (DP), Epsiba Kiwhelu (NCCR- Mageuzi), Mkama Rashid(NRA), Simion Bayo(SAU), Alfred Mollel (UDP) na Elias Sumari(UPDP).

Kampeni za uchaguzi huo zinaanza kesho Jumatano tarehe 26 Agosti 2020 na zitahitimishwa 27 Oktoba 2020 na siku inayofuati itakuwa ni Uchaguzi Mkuu.

1 Comment

  • Nimefurahi kuona wamepiga picha ya pamoja ,lakini wasimamizi was uchaguzi watende haki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!