Jumba la ghorofa saba likiwa limeshaporomoka
Jumba la ghorofa saba likiwa limeshaporomoka

15 wafunikwa na kifusi cha ghorofa, Kenya

KARIBU watu 15 hawajulikani waliko baada ya jumba la ghorofa saba kuporomoka siku ya Jumatatu (jana) usiku, katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, liliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa makundi ya uokoaji yako eneo la mkasa katika kijiji cha Kware Pipeline mtaa wa Embakasi.

Gazeti la Star nchini Kenya lilisema kuwa watu kadha waliokolewa kabla ya jumba hilo kuporomoka.

Waokoaji wakiendelea kutafuta manusura

Walioshuhudia waliliambia gazeti hilo kuwa jumba hilo lilikuwa limeonyesha dalili baada ya nyufa kuonekana kwenye kuta zake.

Jumla ya watu 49 walifariki wakati jumba lingine liliporomoka kufuatia mvua kubwa mwezi Aprili mwaka huu

 

KARIBU watu 15 hawajulikani waliko baada ya jumba la ghorofa saba kuporomoka siku ya Jumatatu (jana) usiku, katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, liliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa makundi ya uokoaji yako eneo la mkasa katika kijiji cha Kware Pipeline mtaa wa Embakasi. Gazeti la Star nchini Kenya lilisema kuwa watu kadha waliokolewa kabla ya jumba hilo kuporomoka. Walioshuhudia waliliambia gazeti hilo kuwa jumba hilo lilikuwa limeonyesha dalili baada ya nyufa kuonekana kwenye kuta zake. Jumla ya watu 49 walifariki wakati jumba…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Hamisi Mguta

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube