Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 13 washinda rufaa za ubunge, 21 watoswa
Habari za SiasaTangulizi

13 washinda rufaa za ubunge, 21 watoswa

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imechambua rufaa zingine 34 za ubunge kati ya hizo, 13 imewarejesha kugombea ubunge, 21 imezikataa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 9 Septemba 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera imesema rufaa hizo 13 zinahusu majimbo ya Singida Magharibi, Madaba. Ilemela, Namtumbo, Bagamoyo, Liwale, Tunduma, Bukene na Kigamboni.

Dk. Mahera amesema, NEC imekataa rufaa saba za wagombea ambao hawakuteuliwa kutoka majimbo ya Singida Magharibi, Bahi, Handeni Vijijini, Madaba, Singida Mashariki, Ileje, Meatu na Bukene.

Amesema, tume hiyo baada ya uchambuzi, imekataa rufaa 14 za kupinga walioteuliwa kutoka majimbo ya Mwanga, Mafinga, Ilala, Manonga, Igunga na Kisesa.

Soma zaidi: NEC yaweka wazi rufaa 55

“Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea ubunge zilizofanyiwa uamuzi na tume kufikia 89.”

“Hii inafuatia taarifa kwa umma iliyotolewa jana tarehe 8 Septemba 2020 ambapo tume ilitangaza uamuzi wa rufaa 55,” amesema Dk. Mahera.

“Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa tume,” amesema

Katika uamuzi wa rufaa hizo 55, tume iliwarejesha wagombea 15 wa ubunge na 40 ikizikataa kati ya hizo 15 ikikubali uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi wa kutowateua na 25 za kupinga kuteuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!